• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brazil yanyeshewa mvua ya magoli 7-1 na Ujerumani

    (GMT+08:00) 2014-07-09 16:08:55

    Ndoto ya Brazil ya kombe la dunia imemalizika kwa njia ya kutia aibu kubwa na ya kikatili, baada ya Ujerumani kuwavuruga vibaya wenyeji hao katika mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia. Dhoruba ilianza kwa Brazil pale Ujerumani ilipoporomosha mvua ya magoli matano ndani ya dakika 29 za mwanzo mbele ya umati ambao haukuamini macho na masikio yao katika uwanja wa Mineirao. Wachezaji wa Brazil wakiwa bado wanamachungu ya kumpoteza mwenzao aliyejeruhiwa Neymar kabla ya nusu fainali, maombolezo hayo yalizidi baada ya kumkosa nahodha wa timu Thiago Silva. Matokeo hayo mabaya kwa timu hiyo mwenyeji ni ya kwanza katika miaka 39, na yameondoa kabisa matumaini ya kufika fainali siku ya Jumapili. Badala yake Ujerumani itakutana na Argentina au Uholanzi ambao watacheza leo huko Sao Paulo. Katika kipindi cha pili cha mauaji hayo kwa Brazil Ujerumani ilihitimisha kwa kuongeza mabao mawili, na baada ya fedheha kubwa mashabiki wa Brazil waliamua kuanza kushangilia kila pasi ya Ujerumani. Matokeo hayo yaliwashtua na kuwaliza mashabiki wengi na wengi waliamua kukimbia muadhara uwanjani kabla hata mechi haijamalizika. Brazil walijua ndoto yao ya kombe la dunia inaweza kumalizika lakini hakuna aliyetarajia kwamba itamalizika namna hii. Katika dakika ya 90 Oscar aliamua kupunguza jazba na machozi ya mashabiki wa Brazil kwa kuingiza goli ambalo halikufaa chochote mbele ya Ujerumani. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalikuwa 7-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako