Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose amevunja rikodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika historia ya kombe la dunia kwa kuingiza goli lake la 16 walipocheza nusu fainali na Brazil. Mshambuliaji huyo wa timu ya Lazio mwenye miaka 36, ameipatia timu yake magoli mawili ya uongozi huku wakiendeleza kuvurumisha magoli na kufikia matano katika kipindi cha kwanza. Klose ambaye alikuwa na magoli sawa na mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo wakati alipoifunga Ghana mapema kwenye michuano hii, sasa ameshampita na kuchukua nafasi ya kileleni kabisa. Mjerumani huyo anayeongoza kwa kufunga magoli mengi, ana jumla ya magoli 71 kwa mechi 136 alizocheza, na ni mchezaji wa tatu kuwa mfungaji bora katika michuano mine ya kombe la dunia. Mchezaji mashuhuri wa Brazil Pele na Yule wa Ujerumani Magharibi Uwe Seeler wote walipata magoli katika michuano ya mwaka 1958, 1962, 1966 na 1970. Ujerumani haijpoteza mechi hata moja ambayo Klose aliingiza magoli.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |