• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waamuzi wa Afrika wateuliwa kuendelea kuchezesha michuano ya kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-07-09 16:09:22

    Timu mbili za waamuzi wa Afrika zimeteuliwa na FIFA kubaki kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha mechi zilizosalia za kombe la dunia zikiwemo, nusu fainali, nafasi ya tatu na mechi ya fainali itakayochezwa Julai 13 katika uwanja wa Maracana. Kamati ya waamuzi ya FIFA juzi ilitangaza hadharani orodha ya timu 15 zenye waamuzi watatu kila moja ambao watabaki Brazil hadi mwisho wa michuano hii. Orodha hiyo ya timu 15 za waamuzi ina timu mbili za wamuzi wa Afrika zinazojumuisha muamuzi mkuu kutoka Ivory Coast Doue Noumandiez, akisaidiwa na Yeo Soguinfolo na Mburundi Jean Claude Birumushahu. Timu nyingine inaongozwa na muamuzi mkuu Haimoudi Djamel kutoka Algeria, akisaidiwa na Redouane Achik (Morocco) and Etchiali Abdelhak (Algeria). Katika mashindano hayo kulikuwa na timu 25 za waamuzi tatu ya hizo ni za Afrika. Miongoni mwa timu 15 za waamuzi waliosalia kuchezesha michuano hiyo yumo refa Mjapani Yuichi Nishimura ambaye alikosolewa sana kwa kuipa zawadi ya penalty Brazil katika mechi ya ufunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako