Naibu mkurugenzi wa Shirika la Afya la Duniani WHO anayeshughulikia usalama wa afya Bw. Keiji Fukuda amesema, maambukizi ya Ebola kwenye nchi za Afrika magharibi yako chini ya udhibiti.
Fukuda amesema hayo mjini Konakry, mji mkuu wa Guinea baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa mawaziri wa afya wa nchi za Afrika Magharibi kuhusu mapambano dhidhi ya Ebola. Fukuda ameipongeza serikali ya Guniea kwa kuchukua hatua zenye ufanisi za kukabiliana na ugonjwa huo zikiwemo kuimarisha usimamizi, kuwatenga wagonjwa, kujenga maabara, na kutoa elimu.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na WHO, hadi kufikia Julai 8, Ebola imesababisha vifo vya watu 518 nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |