• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani watawazwa kuwa mabingwa wa dunia kwa mara nne

    (GMT+08:00) 2014-07-14 16:20:58

    Ujerumani imetawazwa kuwa mabingwa wa dunia kwa mara ya nne, baada ya muda wa kawaida kumalizika bila majibu na kuongezewa muda wa ziada uliozaa matunda kwa mabingwa hao kuwabanjua goli 1-0 Argentina kwenye fainali ya kombe la dunia. Goli hilo liliingizwa na Mario Gotze baada ya kuonesha ufundi maridadi dakika saba tu kabla ya mpira kuingia kipindi cha mikwaju ya penalty. Licha ya Argentina kumchezesha mchezaji mwenye kipaji Lionel Messi, lakini walishindwa kuwajibu wajerumani ambao wamechukua taji kwa mara ya kwanza tangu walipowashinda waargentina haohao huko Rome miaka 24 iliyopita. Mafanikio hayo yanaifanya timu ya Joachim Low kuwa ya kwanza kutoka Ulaya kunyakua taji hilo kubwa duniani katika Amerika Kusini. Ujerumani walilazimika kujipanga vizuri baada ya kumpoteza kiungo wao Sami Khedira kufuatia kujeruhiwa katika mazoezi ya kupasha viungo moto na badala yake nafasi hiyo ikachukuliwa na Christoph Kramer. Ni mafanikio makubwa kwa kocha Low ambaye sio tu ameweza kupeleka kombe nyumbani, bali pia ameondoa rikodi ya Ulaya ya kukosa mataji michuano ianpochezwa katika ardhi ya Amerika Kusini. Wajerumani ambao miaka minne iliyopita walifungwa kwenye hatua ya nusu fainali, sasa wamekamilisha mabadiliko kwa kuwa kikosi chenye wachezaji wanaoibukia kama vile Manuel Neuer, kiungo Mesut Ozil, mlinzi Mats Hummels, nahodha Philipp Lahm, Thomas Muller, Toni Kroos and hata Khedira aliyejeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako