• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha soka cha Brazil kuamua hatma ya Scolari

    (GMT+08:00) 2014-07-14 16:21:42

    Kocha Luiz Felipe Scolari amesema atamuachia rais wa chama cha soka cha Brazil kuamua kama ataendelea kuwa kocha wa Brazil au la. Brazil ilimaliza michuano yake ya kombe la dunia huku ikipata kichapo cha mwaka cha magoli 3-0 walipocheza na Uholanzi katika hatua ya kusaka mshindi wa tatu siku ya jumamosi, siku nne tu baada ya kuvurumishiwa mvua ya magoli 7-1 na Ujerumani kwenye mechi ya nusu fainali. Mkataba wa Scolari unamalizika baada ya kombe la dunia lakini ilidhaniwa kuwa anaweza kuongezewa. Scolari aliiongoza Brazil kupata ushindi mwaka 2002, lakini katika mechi yao ya mwisho wakati jina lake lilipotajwa baada ya kutajwa kikosi cha Brazil, alipokewa kwa kuzomewa huko Brasilia. Wakati mechi hiyodhidi ya Uholanzi ilipokuwa inaendelea kila alipoonekana kwenye skrini uwanjani hapo alizomewa. Kushindwa huko kwenye mechi ya kumsaka mshindi wa tatu inamaanisha kuwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1940, Brazil imeshindwa mechi mbili mfululizo ikiwa nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako