Mji wa Lagos, unaoongoza kwa idadi kubwa ya watu kusini magharibi mwa Nigeria, uko kwenye tahadhari kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola hauingii mjini humo.
Hayo yamesemwa jana na kamishna wa Afya nchini humo, Jide Idris. Kamishna huyo ameshauri watu wazingatie usafi wa binafsi na wa mazingira, ikiwa ni moja ya hatua za kujikinga na kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwenye mkoa huo. Amesema ushauri huo ni muhimu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi na vifo vinavyosababishwa na Ebola katika nchi jirani za Afrika Magharibi kama Guinea, Liberia, na Sierra Leone.
Mji wa Lagos unaongoza kwa idadi ya watu nchini Nigeria ukiwa na jumla ya watu milioni 20, na pia ni mji wa pili unaokua kwa kasi barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |