Rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kufuata hatua zote za kujikinga zinazotolewa na serikali ili kuzuia kutokea kwa matukio ya ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Akiongea kwenye ufunguzi wa hospitali moja mjini Abidjan, rais Ouattar amesema hatua hizo zinaweza kuondoa kwa ufanisi uwezekano wa Ebola kuingia nchini Cote d'Ivoire.
Hivi sasa, ili kukabiliana na uwekezano wa kutokea kwa ugonjwa wa Ebola nchini Cote d'Ivoire, wizara ya afya ya nchi hiyo imetoa amri ya kuimarisha hatua za kusimamia magonjwa ya mlipuko nchini humo, kupiga marufuku watu kula wanyamapori na kuongeza usimamizi juu ya watu wanaoingia na kutoka katika maeneo ya mipaka ya Cote d'Ivoire na Guinea, Liberia na Sierra Leone ambako kumetokea matukio ya Ebola. Mpaka sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kuambukizwa na ugonjwa wa Ebola nchini Cote d'Ivoire.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |