• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israeli yakubali pendekezo la kusimamisha mapigano lililotolewa na Misri

    (GMT+08:00) 2014-07-15 18:24:28

    Baraza la usalama la Israeli leo asubuhi limeamua kukubali pendekezo lililotolewa na Misri kuhusu kusimamisha mapigano yaliyodumu kwa wiki moja sasa katika Ukanda wa Gaza.

    Pendekezo hilo linasema makubaliano ya kusimamisha mapigano yataanza saa 3 asubuhi ya leo kwa saa za huko, na litadumu kwa saa 48. Pande hizo mbili zitaalikwa mjini Cairo, Misri ili kufikia makubaliano kamili. Pendekezo hilo pia limeitaka Israeli kuacha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, na kujizuia kufanya mashambulizi ya ardhini, nalo kundi la Hamas litaacha kurusha makombora ndani ya Israeli.

    Hata hivyo, msemaji wa kundi la Hamas, Sami Abu Zuhri amesema, kundi hilo limekataa mapendekezo ya Misri yanayolenga kusitisha operesheni ya Israeli katika Ukanda wa Gaza, na kusema makubaliano yanatakiwa kufikiwa kwanza. amesema, ardhi ya Palestina bado inakaliwa, na ni haki ya watu wake kujilinda.

    Jumanne iliyopita, Israeli ilianza kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kundi la Hamas na makundi mengine ya wapiganaji mjini Gaza. Wizara ya afya ya Gaza imesema, mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wapalestina 187 na wengine 1,390 kujeruhiwa, na kuharibu nyumba zaidi ya 250.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako