Shirka la ndege la Ethiopia kuanza ziara za moja kwa moja kila siku kwenda London
(GMT+08:00) 2014-07-16 19:54:09
shirikala ndege la Ethiopia Airlines limeanzisha ziara za moja kwa moja za kila siku kati ya Addis Ababa na uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London Uingereza.
Aidha shirika hilo limesema kutakuwa na ziara nyingine pia kutoka London kila jumanne .
Mkurungezi mkuu wa shirika hilo Tewolde Gebremariam alisema London ni mojawepo wa miji muhumu kwa shirika hilo na kwamba litsaidia wasafiri wa kimataifa wanaotumia shirika hilo haswa wafanyi biashara na watalii.
Shirika la ndege la Ethiopia ni miongoni mwa yale tano bora barani Afrika na sasa linahudumu kwenye miji 49 barani humu.