• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa riadha Tanzania Suleiman Nyambui aeleza sababu za kushukiwa kusafirisha dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2014-07-22 11:11:45

    Kocha wa timu ya taifa ya riadha na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amesema aliomba afungwe miaka 100 jela kama ikibainika anajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya. Kocha huyo mpya wa timu ya taifa alisema bado anateswa na 'mzimu' wa kashfa ya kusafirisha dawa za kulevya iliyowahi kumkabili, ambayo iliichanganya familia yake na yeye mwenyewe. Nyambui alisema, katika maisha yake ya riadha tangu akikimbia katika miaka ya 70 hadi hivi sasa akiwa kocha na katibu mkuu, hakuna changamoto kubwa ambayo hataisahau kama siku alipoitwa kuhojiwa juu ya tuhuma hiyo. Kigogo huyo wa RT alisema alijikuta akiingia matatani na kuhojiwa na kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya huko Tanzania kwa saa sita mfululizo juu ya kuhusika kwake na uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. Alisema watu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya walikuwa na vielelezo vyote vya namna RT ilivyohusika kuwaombea visa watu waliokamatwa na dawa za kulevya ambao alikiri yeye ndiye alihusika kuwaombea, lakini hakujua kama ni wauza 'unga'. Watu hao walikuwa wadhamini wa RT na waliwasaidia wanariadha wa Tanzania kwenda Australia kushiriki mashindano ya kimataifa ya kutafuta viwango vya kushiriki Olimpiki ya 2008 hapa Beijing, China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako