• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yataka kutokomezwa ukeketaji na ndoa za utotoni

    (GMT+08:00) 2014-07-23 10:25:23

    Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF zinaonyesha kuwa, ukeketaji na ndoa za utotoni zinaathiri maisha ya mamilioni ya wasichana duniani, na ni lazima kuongeza kasi kwa hatua za kutokomeza desturi kama hiyo.

    Kutokana na takwimu hizo, katika miongo mitatu iliyopita ukeketaji na ndoa za utotoni vimepungua kiasi, lakini kasi ya hatua za kutokomeza desturi hizo inapaswa kuongezwa, ili kulingana na kiwango cha ongezeko la idadi ya watu katika nchi ambazo bado zina desturi hiyo.

    Takwimu zinasema, zaidi ya wasichana na wanawake milioni 130 wamekabiliwa na aina moja au nyingine ya ukeketaji katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya Kati na zaidi ya wanawake milioni 700 walio hai waliolewa wakiwa watoto, milioni 250 kati yao wakiwa na chini ya umri wa miaka 15. Serikali ya Ethiopia jana ilisema itatokomeza ndoa za utotoni na ukeketaji ifikapo mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako