• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Lenovo yatilia maanani shughuli za Internet

    (GMT+08:00) 2014-07-23 12:03:52

    Gazeti la Nikkei la Japan linasema ripoti moja ya uchunguzi wa soko inaonesha kuwa kampuni ya kompyuta ya Lenovo imekuwa kubwa zaidi duniani badala ya Kampuni ya Hewlett Packard. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kampuni ya utafiti wa soko ya Canalys, mauzo ya kompyuta za Lenovo yaliongezeka na kufikia asilimia 12 ya mauzo yote katika soko la kimataifa katika robo ya kwanza ya mwaka huu kutoka asilimia 10 ya mwaka jana wakati kama huu.

    Takwimu zilizotolewa na kampuni ya utafiti wa soko ya Gartner zinaonesha kuwa, kuanzia robo ya tatu ya mwaka 2012, mauzo ya kompyuta za Lenovo yamechukua nafasi ya kwanza duniani badala ya HP. Kampuni ya Lenovo, iliyoanzishwa mwaka 1984, imetumia miaka isiyozidi 30 tu kuwa kampuni kubwa ya sayansi na teknolojia ambayo inashughulikia mambo mbalimbali ya upashanaji habari, na ina uwezo mkubwa wa kufanya uvumbuzi. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yang Yuanqing anasema,

    "Asilimia 60 ya mapato ya kampuni yetu yanatoka nchi za nje, lakini asilimia 60 ya kazi za usanifu zinafanyika hapa China, asilimia 70 ya wafanyakazi wako China, na asilimia 80 ya kazi za utengenezaji zinafanyika China."

    Baada ya kampuni ya Lenovo kutoa mikakati ya kuingia soko la kimataifa mwaka 2001, sasa imekuwa kampuni kubwa zaidi ya kompyuta duniani. Mafanikio yake yanatoka na kununua shughuli za PC za kampuni ya IBM mwaka 2004. Baadaye kampuni ya Lenovo iliingia soko la kimataifa kwa kasi kubwa.

    Mwishoni mwa mwaka 2004, kampuni hiyo ilitangaza kununua hisa za PC za kampuni ya IBM kwa dola za kimarekani bilioni 1.75, na utekelezaji wa kazi ulianza rasmi Mei mosi mwaka 2005. Wakati huo China ilikuwa na muda mfupi tu tangu ijiunge na Shirika la Biashara Duniani, ushuru wa kompyuta ulifutwa, kampuni za kompyuta za China zilikabiliwa na changamoto kubwa. Katika hali hii shughuli za jadi za kampuni ya Lenovo zilikwama, na shughuli mpya hazikupata maendeleo, jambo lililoifanya kampuni hiyo ifanye mageuzi haraka. Wakati kampuni ya IBM iliipotaka kuuza hisa zake, kampuni ya Lenovo bado ilikuwa bado mpya katika soko la kimataifa, na kulikuwa na mazungumzo ya kina kati ya viongozi wa kampuni ya Lenovo kama kampuni hiyo inaweza kununua hisa za kampuni ya IBM au la. Mwanzilishi wa kampuni ya Lenovo Bw. Liu Chuanzhi anasema,

    "Baada ya kujua sababu ya kampuni ya IBM kupata hasara katika shughuli za PC na kuona ni jinsi gani kampuni ya Lenovo inaweza kutatua matatizo mbalimbali, mimi sikutoa amri yoyote, bodi ya kampuni yetu ilipitisha uamuzi wa kununua hisa za PC za kampuni ya IBM."

    Baada ya ununuzi huo, chapa ya IBM, hakimiliki zake, na njia za mauzo za kampuni ya IBM zimeisaidia sana kampuni ya Lenovo kuingia soko la kimataifa, na kuifanya kampuni hiyo ichukue nafasi ya tatu kati ya makampuni makubwa zaidi ya kompyuta duniani. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Chen Xudong alisema,

    "Kununua hisa za kampuni ya IBM kumeongeza umaarufu wa chapa ya Lenovo. Idadi ya wateja wa Marekani wanaonunua kompyuta za Lenovo imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Zamani wateja wasiozidi asilimia 10 walinunua kompyuta za Lenovo, naamini sasa zaidi ya asilimia 50 ya wateja wanazifanya kompyuta za Lenovo kuwa chaguo la kwanza wanaponunua kompyuta."

    Baada ya kuungana na kampuni ya IBM, kampuni ya Lenovo imekuwa kampuni inayofahamika dunia nzima. Bw. Chen anasema,

    "Kampuni yetu imejifunza namna za kufanya biashara katika soko la kimataifa, kusimamia shughuli katika nchi mbalimbali, kutunga mipango ya kimkakati, na kuanzisha utamaduni wa kampuni yetu unaoendana na mahitaji ya soko la kimataifa."

    Ingawa kampuni ya Lenovo imechukua nafasi ya kwanza kati ya makampuni ya kompyuta duniani, lakini katika miaka miwili iliyopita, kutokana na maendeleo ya kasi ya shughuli za mobile Internet, mahitaji ya kompyuta za jadi yamepungua katika soko la kimataifa. Makampuni mengi ya kompyuta, ikiwemo kampuni ya Lenovo, yanakabiliwa na changamoto kubwa. Bw. Yang Yuanqing anasema,

    "Katika miaka kadhaa iliyopita, kampuni yetu ilitilia maanani kazi za kutengeneza chipset na Operating System, lakini sasa wateja hawazingitii mambo hayo mawili, wanapenda zaidi software za simu ya mkononi."

    Bw. Liu Chuanzhi anasema,

    "Baada ya mobile Internet kuanza kutumika, kampuni yetu inayoshughulikia utengenezaji wa kompyuta inakabiliwa na changamoto ya kushirikisha bidhaa zetu na huduma."

    Kampuni ya Takwimu ya Kimataifa imekadiria kuwa, mauzo ya simu za mkononi zenye Operating System au kompyuta aina ya tablet yatafikia bilioni 2.3 mwaka 2017 kutoka bilioni 1.5 mwaka jana. Katika hali hii, kampuni ya Lenovo inahitaji kupata mafanikio zaidi katika simu za mkononi na tablet.

    Mwezi Januari mwaka 2010, kampuni ya Lenovo ilitangaza mikakati yake ya kuendeleza shughuli za mobile Internet mjini Las Vegas Marekani, na kutoa bidhaa mpya za mobile Internet. Hii inamaanisha kuwa, kampuni ya Lenovo ilianza rasmi kushughulikia utengenezaji wa simu za mkononi zenye Operating System au tablet, ili kutafuta fursa mpya za maendeleo na kupata faida kutokana na bidhaa mpya. Bw. Yang Yuanqing anaona kuwa, kampuni yake ina uwezo wa kukabiliana na changamoto mpya, akisema,

    "Kampuni yetu si kama tu imedumisha hali ya kutangulia na kupata faida katika soko la kompyuta, bali pia imeanzisha shughuli mpya, zikiwemo utengenezaji wa tablet, simu za mkononi aina ya smartphone, server na vifaa vya kuhifadhi data. Kuanzisha shughuli mbalimbali kunasaidia kampuni yetu ikabiliwe na changamoto ya kushuka kwa soko la kompyuta. Kampuni yetu inaweza kupata faida nyingi zaidi, na kupata maendeleo endelevu."

    Mwishoni mwa mwaka jana, tablet ziitwazo Yoga zinazotengenezwa na kampuni ya Lenovo zilianza kuuzwa duniani. Mauzo ya tablet hizo katika mwezi wa kwanza tangu zitolewe yalikuwa milioni moja. Naibu meneja mkuu wa kampuni ya Lenono Bw. Chen Xudong alipofahamisha sifa za za aina hii ya tablet anasema,

    "Ukichukua tablet aina ya Yoga mkononi, utaona raha zaidi, na unaweza kuitumia kwa muda mrefu, kwa sababu betri yake inaweza kufanya kazi kwa saa 18. Wateja wengi wanapotumia tablet za chapa nyingine wanaona ni vigumu kuzibeba mkononi, nadhani wakiona tablet zetu, watafurahi sana. Kwa sababu kompyuta yetu haina tatizo hili."

    Kampuni ya Lenovo inaona kuwa, mahitaji ya wateja yanaihimiza ifanye uvumbuzi, idara ya usanifu inatafiti mahitaji ya wateja wa hali tofauti, ili kutengeneza bidhaa zinazowaridhisha zaidi wateja.

    Katika kompyuta ya kiongozi wa kikundi cha usanifu Bw. Cao Peili, kuna mipango makumi kadhaa ya usanifu. Kikundi cha usanifu kimekuwa kinajadili mipango hiyo, na kufuta mipango ambayo haiendani na mahitaji ya wateja.

    Usanifu na utengenezaji wa tablet umebadilisha hali iliyo nyuma ya kampuni ya Lenovo katika soko la mobile Internet. Katika mwaka mmoja uliopita, mauzo ya vifaa mbalimbali yalifikia milioni 115, ambayo inamaanisha kuwa, kila sekunde moja bidhaa tano za chapa ya Lenovo zinauzwa. Hivi sasa Kampuni hiyo imeharakisha usanifu wa tablet aina ya Yoga2, ili kushindana na makampuni ya Apple na Samsung.

    Na katika shughuli za simu za mkononi aina ya Smartphone, kampuni ya Lenovo inapanga kununua hisa za motorola mobile kutoka kampuni ya Google. Kwa mujibu wa mpango huo, kazi hiyo itamalizika mwishoni mwa mwaka huu. Baada ya kazi hii kumalizika, kampuni ya Lenovo itachukua nafasi ya tatu duniani badala ya kampuni ya Huawei.

    Mkurugenzi msaidizi wa utafiti wa tawi la China la Kampuni ya Takwimu ya Kimataifa Bw. Wang Jiping anasema,

    "Kampuni ya Lenovo imechukua nafasi ya kwanza kati ya makampuni ya simu za mkononi ya China katika soko la China, lakini haijaanzisha shughuli zake katika soko la kimataifa. Kampuni hiyo ikinunua hisa za Motorola, itaweza kuingia masoko ya Amerika Kaskazini, Latin Amerika, Ulaya ya Kati na Ulaya Mashariki kwa kasi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako