• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masanduku meusi ya ndege namba MH17 yawasili nchini Uingereza

    (GMT+08:00) 2014-07-23 19:40:08

    Masanduku mawili meusi ya ndege namba MH17 ya Shirika la Ndege la Malaysia yamewasili nchini Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi. Taarifa iliyotolewa leo na kamati ya uchunguzi ya serikali ya Ukraine imesema, Ukraine haikutoa taarifa yoyote kutoka kwenye masanduku hayo kabla ya kuyakabidhi kwa wataalam wa kimataifa.

    Masanduku hayo yanayorekodi taarifa zote za ndege hiyo yamepelekwa kwenye maabara huko Farnborough, magharibi mwa Uingereza, chini ya usimamizi wa wataaalamu wa shirikisho la kimataifa la usafiri wa anga, ICAO.

    Alhamis iliyopita, ndege namba MH17 aina ya Boeing 777 ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyokuwa ikitokea Amsterdam kuelekea Kulala Lumpur, ilianguka karibu na mji wa mashariki wa Ukraine wa Donetsk, na kusababisha vifo vya abiria wote 298 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako