• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya power yapokea mkopo wa kuunganisha wateja zaidi na stima

    (GMT+08:00) 2014-07-23 20:08:05

    Kenya- Kampuni ya kawi nchini kenya-Kenya Power inatarajiwa kupokea mkopo wa shilingi bilioni 3.6 kutoka shirika la maendeleo la Ufaransa AFD na umoja wa ulaya fedha ambazo zitatumika kuunganisha stima kwa wateja 300, 00o.

    Mradi chini ya mpango wa Stima Loan utatekelezwa ndani ya miaka 4 ijayo.Meneja mkurugenzi wa kenya power Ben Chumo anasema sehemu ya kwanza ya fedha hizo ambazo ni milioni 480 zitatolewa ndani ya miezi miwili.

    Chumo alisema mpango huo wa Stima Loan tayari ulikuwa ulifanikiwa kwenye awamu ya majaribio ilioanza mwaka wa 2010 na kufaidi zaidi ya watu 50, 000 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako