• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapokea dola milioni 122 za kuimarisha elimu.

    (GMT+08:00) 2014-07-23 20:09:14

    Tanzania- Benki ya dunia imeipa Tanzania ruzuku ya dola milioni 122 za kuboresha elimu kwenye shule za msingi na za upili.

    Wakurugenzi wakuu wa benki hiyo pia wameidhinisha msaada zaidi kwa mradi unaoendelea wa sayansi na teknolojia ambao unalenga kuongeza ujuzi na utenda kazi wa wanafunzi.

    Fedha hizo zimetolewa chini ya mpango wa Big Results Now ulianzishwa ili kuboresha matokeo na ujuzi wanaopata wanafunzi shuleni.

    Sekta ya elimu nchini Tanzania imekumbwa na changamoto katika miaka ya nyuma zikiwemo ukosefu wa fedha za kutosha kufadhili maabara za sayansi kwenye shule za upili.

    Taakwimu zilizotolewa hivi karibuni na benki hiyo zinaonyesha kwamba kila mwaka wanafunzi 800, 000 huitimu kutoka vyuoni lakini wengi wao hawana ujuzi unaohitajika na waajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako