Shirika kubwa la ndege nchini Nigeria, Arik Air, limesitisha safari za ndege zake kuelekea Monrovia, mji mkuu wa Liberia, na mji wa Freetown nchini Sierra Leone kutokana na kugundulika kwa mgonjwa wa kwanza mwenye maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola mjini Lagos.
Ijumaa iliyopita, serikali ya Nigeria ilithibitisha kuwa, raia mmoja wa Liberia aliyewasili nchini humo wiki moja kabla, amefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola mjini Lagos, na kuwa mgonjwa wa kwanza kuwa na maambukizi hayo nchini Nigeria.
Shirika la Afya Duniani limesema, watu 660 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola katika nchi tatu za Guinea, Liberia, na Sierra Leone.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |