• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza na Afrika Kusini zachukua tahadhari dhidi ya virusi vya Ebola

    (GMT+08:00) 2014-07-31 10:55:39

    Serikali ya Uingereza jana iliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kujadili kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. Wizara ya afya ya Afrika Kusini jana pia ilitangaza nchi hiyo kuingia katika hali ya tahadhari, ili kuzuia virusi vya Ebola kuingia nchini humo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Philip Hammond amesema, hadi sasa hakuna raia wa Uingereza aliyeambukizwa virusi hivyo, lakini waziri mkuu Bw. David Cameron anaona ni lazima kuchukua tahadhari kwa makini kuhusu ugonjwa huo.

    Waziri wa afya wa Afrika Kusini Bw. Aaron Motsoaledi amesema, kutokana na kuenea haraka kwa virusi vya Ebola katika baadhi ya nchi za Afrika magharibi, Afrika Kusini inapaswa kuchukua hatua za lazima za kinga, lakini hakuna haja ya kuwa na hofu, kwani Afrika Kusini ina "njia yenye ufanisiya usimamizi na udhibiti".

    Kulikuwa na habari kuwa mwanamke wa Hongkong aliyerudi kutoka Afrika aligunduliwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, lakini msemaji wa Shirika la Afya Duniani WHO Paul Garwood amesema, ingawa hali ya ugonjwa wa Ebola katika Afrika magharibi ni mbaya, watu wa China hawana haja kuwa na hofu.

    (adela fadhili hasani)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako