• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Jamii Bora kufadhili uunganishaji wa umeme

    (GMT+08:00) 2014-07-31 19:28:48
    Kampuni ya umeme ya Kenya na Benki ya Jamii Bora zimesaini mkataba ambao utapelekea wateja wapya wanaotaka kuunganishwa na umeme kupata mkopo. Kupitia mkataba huo,kampuni ya umeme ya Kenya inatarajia kuongeza idadi ya uunganishaji mpya katika juhudi za kufikia malengo ya serikali ya watu zaidi ya asilimia 70 kupata huduma za umeme katika miaka mitano ijayo. Mkopo huo utahudumia wateja wa makundi yote,ikiwa ni pamoja na wale wanaotaka mita za awamu moja zinazotumika sana manyumbani ,na za awamu tatu zinazotumika kwa biashara. Akizungumza jana wakati wa kutiwa saini kwa mkataba huo,Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya umeme Kenya Ben Chumo alisema kwa kupewa mkopo wateja wao wataweza kupata huduma za umeme.Alisema anatarajia wakenya kuchukua mkopo huo hasa maeneo ya vijijini ambako kuna changamoto katika kupata pesa. Hata hivyo kampuni ya umeme ya Kenya haikuweka wazi idadi ya wateja wapya waliolengwa chini ya mkataba huo,lakini kulingana na Chumo wateja 453,000 waliunganishwa mwaka jana. Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Jamii Bora Samuel Kimani alisema watu wote wataunganishwa na mita mpya za kulipia kwanza ili kuepuka hatari ya kutolipia umeme. Benki hiyo itatoa mkopo kwa kiwango cha riba cha asilimia 16 kwa wateja wote. Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya umeme ya Kenya kushirikiana na taasisi za kifedha kutoa mikopo ili kufadhili uunganishaji wa umeme. Wiki iliyopita kampuni hiyo ilisema imeingia mikataba na Benki ya Equity na ile ya National kwa ajili ya ufadhili wa uunganishaji umeme.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako