• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duka kubwa la uchumi laanza shughuli za masaa 24 Dar

    (GMT+08:00) 2014-07-31 19:29:35
    Wenye kufanya manunuzi usiku jijini Dar es Salaam sasa wana sababu ya kufurahia kufuatilia kufunguliwa kwa duka kubwa la Uchumi. Kampuni hiyo ya maduka makubwa ya reja reja jana ilifungua tawi lake jipya la Makumbusho katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi ambalo litakuwa wazi masaa 24. Hatua hiyo inahusishwa na kuongezeka kwa mahitaji ya wateja.Meneja wa Uchumi nchini Tanzania Chris Lenana alisema kuongezeka kwa mahitaji ya wateja,hasa katika matawi ya Makumbusho na Shekilango kumelazimisha kampuni hiyo ya maduka makubwa ya reja reja kuanzisha huduma za masaa 24. Alisema kuwa ana furaha kuwaambia wateja wao kuwa sasa wanaweza kununua bidhaa katika matawi hayo mawili wakati wowote wanaotaka. Hatua hiyo imekujua wakati mpinzani wao Nakumatt ilifungua duka katika tawi la Mlimani City jumapili iliyopita. Uchumi iliingia katika soko la Tanzania mapema mwaka 2012 na hivi sasa inaendesha maduka mannne makubwa ya reja reja. Kampuni hiyo pia inatarajia kufungua matawi sita zaidi kabla ya mwaka kuisha:matawi matatu jijini Dar es Salaam,moja mjini Arusha,Morogoro na Mwanza. Meneja wa Uchumi Chris Lenana amesema kuwa biashara inanoga na inahitaji kupanuliwa,kwa lengo la kupeleka huduma karibu na wateja.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako