• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO na nchi za Afrika Magharibi kuzindua mpango wa kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-01 10:39:13

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Afya Duniani WHO Bibi Margaret Chan na marais wa nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na mlipuko wa homa ya Ebola za Guinea, Liberia na Sierra Leone, leo wanakutana nchini Guinea kuzindua mpango mpya wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 100 kupambana na ugonjwa huo. Nchi hizo zimeeleza matakwa yao ni nini na WHO itawasiliana na jumuiya ya kimataifa ili kutekeleza mpango huo.

    Wakati hali ya ugonjwa huo ikiendelea kufuatiliwa katika sehemu mbalimbali duniani, wizara ya afya ya Uganda imekanusha ripoti kuwa mtu mmoja ameambukizwa homa ya Ebola nchini Uganda. Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bw Ruhakana Rugunda amesema vipimo vinaonesha kuwa mtu aliyedhaniwa ameambukizwa hakuambukizwa.

    Marekani pia imetoa tahadhari kwa maofisa wake kutofanya safari zisizo muhimu kwenda Guinea, Liberia na Sierra Leone na kutoa tahadhari ya ngazi ya tatu. Hata hivyo Ikulu ya Marekani imesema mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika utafanyika wiki ijayo kama ilivyopangwa, licha ya nchi za Afrika Magharibi kukumbwa na homa ya Ebola.

    Habari nyingine zinasema kuwa, msemaji wa shirika la WHO Bw. Gregory Hartl amesema, hivi sasa uwekezano wa kutokea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nje ya kanda ya Afrika magharibi sio mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako