• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baada ya msanii wa Tanzania AY kutembelea white house aeleza kilichomvutia

    (GMT+08:00) 2014-08-05 10:44:22

    A.Y na wasanii wenzake wapo nchini Marekani na wameanza kwa kukutana na Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval. Msafara huu wa wasanii kutoka Afrika unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y ambapo leo wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama. Baada tu ya kufika, Ay amesema kitu tofauti alichokutana nacho kwenye Ikulu hiyo ni kwamba wafanyakazi wanakwenda na mavazi maalumu kutokana na siku, yaani yamepangwa mavazi ya kuvaa kutokana na siku, kwa weekend ambayo Ay na wenzake waliitembelea Ikulu mtu yeyote haruhusiwi kuvaa suti hivyo waliwakuta wafanyakazi wengine wakiwa wamevaa kaptula au jeans. Alisema hata wao pia wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend. Ay anasema kingine ni kwamba Obama kila wiki anatenga siku ya kukutana na Watoto kutoka sehemu mbalimbali wanaotembelea Ikulu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako