Nchi za kusini mwa Afrika zinatarajia kufanya mkutano kuhusu njia za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola endapo utatokea kwenye kanda hiyo.
Katibu mkuu wa wizara ya afya nchini Zambia David Chikamata amesema, maandalizi ya mkutano wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao umeleta maafa makubwa kwa nchi za Afrika magharibi yanaendelea.
Gazeti la Zambia Daily limemnukuu Chikamata akisema, mkutano huo utakaozihusisha nchi za Zimbabwe, Zambia, na Malawi, ni muhimu na utazisaidia nchi husika kubadilisdhana maoni kuhusu njia za kukabiliana na ugonjwa huo hatari. Hata hivyo katibu mkuu huyo hakusema mazungumzo hayo yatafanyika lini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |