• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xavi Hernendez astaafu soka ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2014-08-06 10:38:58

    Kiungo wa Barcelona na Hispania Xavi Hernandez ametangaza kustaafu soka ya kimataifa. Hernandez mwenye umri wa miaka 34 alichezea timu yake ya Hispania na kutwaa ushindi na pia makombe mawili ya mabingwa wa Ulaya akiwakilisha nchi yake. Xavi aliwaambia waandishi wa habari Barcelona jana jumanne kuwa amefurahia kucheza soka kwa kipindi chote hadi anapofikia kustaafu. Alianza kung'ara baada ya kuipatia ushindi timu yake ya Hispania katika mechi ya November 15 mwaka 2000 dhidi ya Uholanzi ambayo waliilaza kwa bao1-0, akiwa na umri wa miaka 20. Xavi alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2008 katika ligi ya ulaya wakati ambao Hispania ikimaliza kiu yake ya miaka 44 kutwa kikombe cha kimataifa na kuanza kung'ara duniani. Xavi mwenyewe pamoja na kutangaza kustaafu sasa amesema kuwa ilikuwa hatua hiyo aichukue mwaka 2012 baada tu ya ligi ya Ulaya lakini kocha wake Vicente Del Bosque alimsihi asistaafu hadi baada ya kombe la dunia jambo ambalo ni la kuvunja moyo kwake na kwa wengine pia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako