• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yathibitisha wagonjwa 8 wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-06 20:24:39

    Kamishna wa afya wa jimbo la Lagos, Nigeria Jide Idris amesema, kuna wagonjwa 8 wanaoshukiwa kuwa na virusi ya Ebola jimboni humo. Idris amesema, watu hao waliwahi kuwa karibu na Patrick Sawyer, ambaye ni raia wa Liberia aliyefariki kutokana na virusi hiyo mwezi uliopita.

    Kwa mujibu wa Idris, sita kati ya watu hao wamewekwa kwenye wodi maalum, lakini bado hawana dalili yoyote ya virusi hiyo. Ameongeza kuwa, serikali inachukua hatua kutafuta wengine wote waliokuwa karibu na raia huyo wa Liberia.

    Waziri wa afya wa Nigeria Onyebuchi Chukwu amethibitisha kuwa muguzi mmoja aliyemtibu mgonjwa mmoja wa Ebola amefariki baada ya kuambukizwa virusi hiyo jimboni Lagos. Lakini haijajulikana kama muuguzi huyo ni mmoja kati ya watu hao wanne wanaoshukiwa kuambukizwa na virusi hiyo.

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema, mpaka sasa watu 1,603 wameambukizwa virusi hiyo, ambapo 887 wamefariki katika nchi za Guinea, Liberia, Nigeria na Sierra Leone.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako