• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liberia na Nigeria zatangaza hali ya hatari kutokana na ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-07 19:14:08

    Liberia na Nigeria zimetangaza hali ya hatari kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, ugonjwa hatari ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 900 mwaka huu katika nchi nne za Afrika magharibi.

    Taarifa rasmi iliyotolewa jana na rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia imesema, serikali na wananchi wa Liberia wanatakiwa kuchukua hatua za ziada kuilinda nchi na wananchi wake. Naye waziri wa afya wa Nigeria Onyebuchi Chukwu amesema, kila mtu duniani kwa sasa yuko kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

    Watu 1,711 wameambukizwa virusi vya Ebola, na wengine 932 wamefariki mwaka huu katika nchi za Guinea, Liberia, Nigeria, na Sierra Leone, katika mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa huo ambao haujatokea kwa karibu miaka 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako