• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatangaza hali ya dharura ya kimataifa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-08 18:57:43

    Shirika la Afya Duniani WHO leo limetangaza kuwa, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika kuwa ni hali ya dharura ya kiafya kimataifa.

    Baada ya mikutano miwili ya kamati ya dharura iliyoitishwa na mkurugenzi mtendaji wa WHO Bi. Margaret Chan chini ya kanuni za afya ya kimataifa, kamati hiyo imeshauri kuwa, mlipuko wa Ebola ni wa aina ya kipekee na ni hatari kwa afya kwa nchi nyingine. Shirika hilo litaitisha mkutano wa wataalam katika fani ya madawa kuchunguza matumizi ya dawa za majaribio ya tiba ya ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika magharibi.

    Habari nyingine zinasema, naibu mkurugenzi wa wizara ya afya ya Benin Aboubacar Moufililatou amesema, mgonjwa mmoja kutoka Nigeria mwenye dalili za mtu mwenye maambukizi ya Ebola amelazwa hospitali mjini Port Novo, Benin.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako