• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yairarua Manchester City kwa magoli 3-0

    (GMT+08:00) 2014-08-11 15:37:48

    Arsenal jana walituma salamu kwa klabu nyingine kwamba msimu huu wameingia kivingine kwa kuonesha mchezo safi sana ulioshia kuisarambatisha Manchester City kwa magoli 3-0 katika uwanja wa Wembley. Washindi hao wa kombe la FA wameanza kuongoza kwenye mechi hiyo kupitia goli la Santi Carzorla, na kuongeza la pili kupitia Aaron Ramsey katika kipindi cha kwanza. Naye Giroud akipigilia msumari kwa kuongeza goli la tatu katika dakika ya 60. Ushindi huo kwa kambi ya Arsene Wenger ni wa kwanza katika ligi ya Uingereza tangu mwaka 2004. Arsenal imewachezesha wachezaji wake watatu kati ya wanne iliyowasanii hivi karibuni, wachezaji hao ni pamoja na mshambuliaji Alexis Sanchez, mlinzi wa kulia Mathieu Debuchy na mlinzi Calum Chambers. Kwa upande wa Man City imekosa wachezaji wake muhimu wanane na wakati kocha Manuel Pellegrini akishuhudia kichapo, hiyo itakuwa ni onyo kwake kabla ya kuanza safari ya kutetea ubingwa wake wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako