• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Promota wa mchezo wa ngumi asema amebadilisha jinsia

    (GMT+08:00) 2014-08-11 15:38:12

    Promota wa zamani wa ndondi Frank Maloney amebainisha kuwa yupo kwenye mchakato wa kubadilisha jinsia na hivi sasa anaishi akiwa kama mwanamke aitwaye Kellie. Katika mahojiano na gazeti la Mirror Kellie amesema alizaliwa katika mwili sio na siku alikuwa anajua kama yeye ni mwanamke. Kellie kwa sasa anafanyakazi na kundi la jinsia la TG Pals. Akiwa kama Frank Maloney alimuongoza Lennox Lewis hadi kupata mkanda wa uzito wa juu wa dunia mwaka 1993. Kellie amesema hakuweza kumwambia mtu yeyote katika tasnia ya ndondi kuhusu nia yake lakini amekuwa akijiandaa kujibadilisha wakati bado akiwa anaishi kama Frank huku akiwa kwenye michezo. Ameeleza kuwa alikuwa na uhakika kuwa angeweza kufanya kazi yake katika mchezo wa ndondi akiwa mwanamke, lakini sasa analenga zaidikusaidia watu wengine wenye matatizo kama yake. Kellie ambaye aliolewa mara mbili na kuwa na watoto, amesema anakusudia kuishi bila mume na sasa anjiandaa kiakili kwa maisha yake yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako