• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gyan awapiku kina Eto'o kwa mapato mengi

    (GMT+08:00) 2014-08-11 15:38:37

    Straika wa Ghana, Asamoah Gyan amewapiku Yaya Toure wa Ivory Coast na Samuel Eto'o wa Cameroon kwa kuwa mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi Afrika. Gyan anaweka kibindoni Dola milioni 16 kwa mwaka kama faida kutoka kwenye mshahara wake na malipo ya mikataba mingine pamoja na biashara zake binafsi. Staa huyo anayecheza soka Falme za Kiarabu mshahara wake haukatwi kodi jambo linalomfanya kuwa na pesa nyingi akimzidi Toure anayeingiza Dola milioni 15. kwa mwaka kutoka kwenye mshahara wake wa Dola laki 3 na 22,000 kwa wiki anaolipwa Manchester City. Samuel Eto'o mshahara wake ni Dola milioni 13.3 kwa mwaka, wakati Emmanuel Adebayor anashika namba nne. Gyan amewekeza pesa zake kwenye vyakula na nyingine ameziwekeza kwenye nyumba, masumbwi, muziki na elimu. Wakati huohuo Didier Drogba ambaye amejiunga tena na club ya Chelsea baada ya kuondoka kwenye club hiyo kipindi kilichopita amegonga tena vichwa vya habari. Drogba amekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast kwa miaka 8 na kucheza kama mchezaji kwa miaka 12. Hivi sasa ametangaza kustaafu kuchezea soka timu ya taifa. Didier akitangaza uamuzi huo alisema, "Ni masikitiko sana kwa kuamua kustaafu kucheza soka na timu ya taifa. Amesema Kuanzia mara yake ya kwanza alivyoitwa kucheza timu ya taifa hadi mechi yake ya mwisho siku zote alijaribu kutoa kilicho bora kwa ajili ya nchi yake. Ameeleza kuwa anajivunia kuwa nahodha kwa miaka 8 na kuchangia kuiweka nchi yake kwenye kiwango cha dunia kwenye soka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako