• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Okwi wa Uganda ana mpango wa kuikimbia Yanga ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-08-11 15:38:53

    Matumaini ya mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza kubaki Tanzania yamefufuka baada ya klabu mbili kumhitaji straika Emmanuel Okwi. Awali Yanga ilikuwa katika hesabu za kumtema Kiiza na kutaka kumbakiza Okwi ingawa uongozi wa Yanga haukuwa na furaha na usumbufu wa Okwi, lakini walilazimika kuamua hivyo kutokana na gharama za kuvunja mkataba wake wa miaka miwili kuwa kubwa tofauti na ule wa Kiiza. Akizungumza akiwa kwao Uganda, Mwanasheria wa Okwi, Edgar Aggaba, alisema Okwi anagombewa na klabu mbili za Ulaya. Aggaba alisema klabu hizo zinatoka katika nchi za Australia na Sweden. Alisema Okwi hawezi kwenda Tanzania sasa, kuna mambo wanayashughulikia, kwani kuna klabu mbili za Ulaya zinataka kumsajili na wapo tayari kuwapa fedha nyingi Yanga kama wakikubali kumtoa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako