• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa afya wa China waenda Afrika Magharibi kushiriki kwenye mapambano dhidi ya Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-11 17:05:29

    Ugonjwa wa Ebola uliozikumba baadhi ya nchi za Afrika Magharibi unafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Wataalamu wa afya waliotumwa na serikali ya China wameondoka kuelekea Guinea, Liberia na Sierra Leone kusaidia kazi ya kupambana na ugonjwa huo. Hii ni mara ya kwanza kwa China kutuma vikundi vya watalaamu wa afya kupambana na ugonjwa huo. Fadhili Mpunji anatueleza zaidi.

    Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti maradhi cha China Bw. Wang Yu alipohojiwa na waandishi wetu wa habari amesema kikundi cha kwanza cha watalamu kiliondoka jana usiku kwenda Guinea, na kitatoa msaada wa kiufundi kwenye kudhibiti ugonjwa wa Ebola, akisema,

    "Wataalamu tisa wakiwa kwenye vikundi vitatu wamekwenda Guinea, Sierra Leone na Liberia. Wana taaluma mbili, ambazo ni matibabu ya ugonjwa na kinga ya maambukizi."

    Mtalaamu Bw Sun hui alikwenda Guinea jana usiku, alipohojiwa kabla ya kuondoka, alisema,

    "Kazi zetu muhimu ni kuusaidia ubalozi kugawa misaada, kuwafundisha wataalamu wa huko kutumia misaada hiyo kwa usahihi, kuwasiliana na vikundi ya matibabu ya China, na kutoa mafunzo ya kukinga na kudhibiti magonjwa kwa wafanyakazi wa ubalozi na makampuni ya China ya huko."

    Virusi vya Ebola ni moja kati ya virusi vinavyosababisha vifo vingi. Hadi sasa kati ya watu 1800 walioambukizwa, 961 wamefariki, hadi sasa bado hakuna dawa au chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Shirika la Afya duniani linauchukulia ugonjwa huo kuwa tukio la dharura la afya linalofuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Licha ya kutuma wataalamu wa afya, serikali ya China pia imetoa vitu vya matibabu vyenye thamani ya yuan milioni 1 kwa kila nchi kwa Guinea, Liberia, Sierra Leone na Guinea Bissau, na kutoa vitu vya msaada wa kibinadamu vyenye thamani ya jumla ya yuan milioni 30 kwa nchi tatu. Vitu vya msaada vimepelekwa huko kwa ndege jana usiku, ambavyo ni kundi la pili la vitu vya msaada linalotolewa na China kwa nchi zenye hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola.

    Vitu hivi ni pamoja na vifaa vya kujikinga, dawa za kuua vijidudu na dawa za kutibu ugonjwa, ambavyo vinahitajiwa sana katika nchi hizo tatu. Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti maradhi cha China Bw. Wang Yu amesema,

    "Kukinga virusi vya Ebola kunahitaji vifaa maalum, ikiwemo barakoa, miwani na nguo maalum, mahitaji ya vitu hivi ni makubwa."

    Sasa vikundi vya matibabu vya China vinnavyofanya kazi nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone vina majukumu yao.

    Mkurugenzi wa idara ya uenezi ya kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Bw. Mao Qun'an amesema wataalamu wa afya wa watafanya juhudi kadri wawezavyo kutoa uungaji mkono wa kiufundi kwa nchi zinazokumbwa na ugonjwa huo, akisema,

    "Hivi sasa ugonjwa wa Ebola bado haujadhibitiwa vizuri katika nchi za Afrika Magharibi, China inapenda kutoa uungaji mkono wa kiufundi kwa nchi hizi, ukiwemo uzoefu wa China katika kupambana na maambukizi makubwa ya dharura ya ugonjwa. Wakati huo huo, China imewataka wataalamu wa afya wanaokwenda Afrika kuonesha moyo wa upendo, na kufanya juhudi kuzisaidia nchi husika za Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako