• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester City yamsaini Eliaquim Mangala kwa pauni milioni 32

    (GMT+08:00) 2014-08-12 19:20:12

    Manchester City imemsaini mlinzi Eliaquim Mangala kutoka klabu ya Porto kwa ada ya pauni milioni 32. Mchezaji huyo mwenye miaka 32 ambaye ni mfaransa amesaini dili la miaka mitano. Kocha wa City Manuel Pellegrini amesema mchezaji huyo ana kila aina ya sifa ya kuweza kuwa miongoni mwa walinzi bora katika Ulaya. Mangala alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichocheza kombe la dunia, lakini hakucheza mechi hata moja. Mangala ni mchezaji wa sita kusainiwa katika klabu ya City na ni wa pili kutoka Porto baada ya kiungo kutoka Brazil Fernando kujiunga na City kwa ada ya pauni milioni 12. Mangala ameanza kibarua chake akiwa na Standard Liege mwaka 2008, na kushinda ligi katika msimu wake wa kwanza, kabla ya kujiunga na Porto mwaka 2011.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako