Mshiriki wa mbio za baiskeli Kris Cook amefariki dunia baada ya kuanguka alipokuwa kwenye mbio za RideLondon zilizofanyika London na Surrey. Cook mwenye miaka 36, alikutwa na mauti baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Jumapili alipokuwa Newlands karibu na Guildford kwenye mbio hizo za RideLondon. Waandaaji wa mbio hizo wamesema alianza kutibiwa na madaktari katika eneo la tukio na kisha kupelekwa hospitali lakini baadaye alifariki. Maelfu ya watu wameshiriki kwenye mbio hizo ambazo zimepunguzwa umbali kutoka maili 100 hadi 86 kutokana na tahadhari hali ya hewa. Msemaji wa Prudent RideLondon amesema Kris alikuwa ni miongoni mwa kundi la waendesha baiskeli 12 ambalo linachangisha pesa kwaajili nyumba ya kuwahudumia wagonjwa mahututi ya Woking. Mama yake amesema mwanawe amefariki akiwa anafanya kitu akipendacho na kukaribisha michango ili kumkumbuka Kris kwa kazi yake ya kuchangisha pesa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |