Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema anamatumaini makubwa kuwa timu hiyo italitetea taji lake licha ya kuambulia kichapo cha mabao matatu kwa nunge dhidi ya mahasimu wao Arsenal katika mechi ya kuwania ngao ya Community iliyochezwa jumapili. Man City, wamepangwa kufungua kampeni ya kutetea taji lao dhidi ya Newcastle jumapili ijayo. Pellegrini alisema sababu ya kufanya vibaya katika mechi hiyo ya jumapili ni kutokuwepo kwa mshambuliaji wake machachari Sergio Aguero mlinzi Vincent Kompany, Pablo Zabaleta na Bacary Sagna jambo ambalo liathiri mchezo huo na kwamba kikosi kilichocheza hakikuwa kikosi chao cha kwanza. Pellegrini alimpa nafasi ya kuanza mchezaji mpya Willy Caballeroin na akamwelezea kipa nambari moja msimu uliopita Joe Hart, kuwa lazima adhihirishe uwezo wake msimu huu kwani ana upinzani mkali.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |