Manchester United imewaonya mashabiki wake wote kwamba hawataweza kuingia na Ipad au simu zozote za tablet ndani ya uwanja wa Old Trafford katika msimu huu. Kumekuwa na tabia ya mashabiki kurikodi mechi kupitia simu za Apple na klabu inawasiwasi kuhusu kutofuta sheria za hakimiliki. United sasa imewaonya mashabiki kuhusu sera zao mpya kupitia barua pepe, kufuatia mechi ya kirafiki iliyochezwa jana usiku dhidi ya Valencia. Barua pepe hiyo imeandikwa " tunataka kuwafahamisha kuhusu sera mpya za klabu kuhusiana na mechi za nyumbani. Mashabiki hawaruhusiwi kuingia na vifaa vikubwa vya elektroniki vyenye ukubwa wa mm150 kwa 100 ndani ya uwanja."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |