Togo inataka mechi ya kombe la Matiafa ya Afrika iliyopangwa kufanyika mwezi ujao nchini Guinea ihamishiwe nchi nyingine kutokana na hofu ya virusi vya Ebola. Mechi hiyo imepangwa kufanyika septemba 5 au 6 na ipo kwenye raundi ya kwanza ya makundi. Zaidi ya watu 300 wamefariki nchini Guinea kutokana na ugonjwa wa Ebola. Shirikisho la Soka la Togo TFF limesema linaogopeshwa na hali hiyo. TFF imesema itafuata ushauri wa serikali yake, ambapo huenda wakazuia kikosi kwenda Guinea. Sierra Leone nayo tayari imeshatangaza kuwa haitaruhusu mechi zozote kufanyika nchini humo hadi litakapotolewa tangazo kwasababu ya ugonjwa huo. Hadi sasa CAF bado haijajibu ombi la Togo na Sierra Leone kuchezea mechi nchi nyingineambayo haijaathirika na Ebola. Hata hivyo mechi ya nje ya nchi ambazo zitazishirikisha Guinea na Sierra Leone zitakuwa na matatizo baada ya Shelisheli kuzuia kikosi cha Sierra Leone kuingia nchini mwake mwezi uliopita kutokana na wasiwasi wa kupeleka virusi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |