Mwenyekiti wa Shirikisho la mchezo wa chess la Angola Bw. Aguinaldo Jaime amechaugliwa kuwa makamu wa rais wa Shirikisho la mchezo huo duniani FIDE huko Tromso, Norway. Rais wa shirikisho hilo Kirsan Ilumzhinov, ambaye ameongoza kwenye uchaguzi huo kwa kupata kura 110 na kuongoza kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2018, amempa nafasi ya makamu wa rais Jaime. Bingwa wa zamani wa chess Garry Kasparov ameshindwa kwa mara ya pili baada ya kupata kura 61. katika uongozi huo mpya Kirsan Ilumzhinov amekuwa rais, Georgios Makropoulos, naibu rais, Abraham Tolentino katibu mkuu, Aguinaldo Jaime makamu wa rais, Martha Fierro Baquero, makamu wa rais na Adria Siegel mshika fedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |