• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa misaada ya matibabu yenye ufanisi kwa wakati kwa nchi za Afrika zinazokumbwa na ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-13 16:27:19

    Mshauri wa rais wa Nigeria ambaye pia ni chifu mwenye asili ya China Bw. Hu Jiegou, amesema serikali ya China imetoa misaada mingi ya vitu vya kinga na matibabu kwa wakati kwa nchi za Afrika Magharibi zinazokabiliwa na ugonjwa wa Ebola, na vikundi vya wataalamu wa matibabu wa China pia vimefika katika nchi hizo, hatua zinazoonesha kuwa China ni nchi kubwa inayowajibika.

    Bw. Hu Jiegou amesema China imekuwa inatuma vikundi vya matibabu barani Afrika kwa muda mrefu, vikundi ambavyo vinasifiwa na wakazi wa huko, akisema,

    "Watu wa Afrika wana matarajio makubwa kuhusu China. China imewekeza kwa wingi barani Afrika, imejenga viwanda na hoteli na kutoa misaada mbalimbali. Hivyo waafrika wanaona ni jambo la kawaida kwa Wachina kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola, Wachina hawawezi kuwasahau watu wa Afrika. Kikundi cha madaktari cha China kimetoa huduma nchini Liberia kwa muda mrefu, sasa China inatoa misaada mingi ya matibabu na kutuma vikundi vya watalamu wa matibabu barani Afrika, hatua hizi zinafurahiwa na waafrika, wanaona China ni rafiki wa jadi wa Afrika. Nadhani serikali ya China imetoa misaada kwa wakati, na China ni nchi kubwa inayowajibika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako