Naibu waziri wa elimu wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa amesema, muhula mpya wa masomo katika vyuo vikuu nchini Ghana utachelewa kuanza kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola.
Akizungumza kupitia redio moja nchini Ghana, Ablakwa amesema kuwa uamuzi huo unalenga kuhakikisha kuwa huduma ya kupima virusi vya Ebola viko tayari kabla wanafunzi kutoka nchi za Afrika magharibi zilizoathiriwa na ugonjwa huo, zikiwemo Nigeria, Liberia, na Sierra Leone kuwasili nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |