• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na Shirika la Afya Duniani wafanya kazi kwa karibu kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-14 10:18:46

    Umoja wa Afrika na Shirika la Afya Duniani WHO wanafanya kazi kwa pamoja kupambana na mlipuko wa homa ya Ebola ambao sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja. Maofisa wa Umoja wa Afrika na WHO wamesema mjini Addis Ababa kuwa pande hizo mbili zinashirikiana vizuri katika kupambana na ugonjwa huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki Moon ameutaka Umoja wa Mataifa uisaidie WHO katika kupambana na Ebola.

    Maofisa wa WHO pia wanasema China imeendelea kuzisaidia nchi zilizokumbwa na homa ya Ebola, na msaada uliotolewa na China umeongeza nguvu katika mapambano dhidi ya homa ya Ebola. Misaada ya China tayari imefikishwa Guinea, Liberia na Sierra Leone. Wataalamu wa China pia wanaendelea kutathmini hatari ya homa ya Ebola na kusema hata kama kutakuwa na mtu aliyeambukizwa hapa China, ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa kwa kuwa China ina uwezo wa udhibiti na kinga ya magonjwa ya kuambukiza.

    Nchi mbalimbali za Afrika zinaendelea na hatua za kuzuia ugonjwa huo. Shirika la ndege la Kenya linapitia upya huduma zake katika nchi za Afrika Magharibi, na Botswana imeweka vizuizi kwa abiria kutoka Afrika Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako