• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi kuisaidia Sierra Leone kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-14 11:03:49

    Hivi sasa ugonjwa wa Ebola ulioanza mwezi Desemba mwaka jana nchini Guinea, na kutajwa kuwa ni "tukio ghafla la afya ya umma linalofuatiliwa na nchi zote duniani", bado unaendelea kuenea na kutishia usalama wa nchi nyingi za Afrika magharibi, mpaka sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja. Katika hali hiyo, misaada ya kibinadamu na wataalam 9 wa afya ya umma waliotumwa na serikali ya China wamewasili Guinea, Sierra Leone na Liberia, ili kuendelea kutoa msaada kwa nchi hizo kupambana na ugonjwa huo. Kwenye sherehe ya kukabidhi msaada, naibu waziri wa mambo ya nje wa Sierra Leone bibi Ebun Strasser-King amesema, msaada uliotolewa na serikali ya China katika hali ngumu ya sasa, utakumbukwa daima na serikali ya Sierra Leone na watu wake.

    Hii ni mara ya pili kwa serikali ya China kutoa msaada kwa nchi za Afrika tangu ugonjwa wa Ebola ulipolipuka barani Afrika. Konsela wa biashara wa China nchini Sierra Leone Bw. Zou Xiaoming alipohojiwa na waandishi wa habari amesema, kutokana na utabiri kuhusu hali ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini Guinea, mwezi Mei China ilitoa pendekezo la kutoa msaada kwa Sierra Leone, wakati ule Sierra Leone ilikuwa haijatoa ombi la msaada. Bw. Zou amesema,

    "Tarehe 13 mwezi Mei shehena zetu zenye thamani ya yuan milioni moja zimesafirishwa kwa Sierra Leona kwa ndege, tarehe 15 tumekamilisha utaratibu wa kukabidhiana, tarehe 16 mgonjwa wa kwanza alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini humo. Hivyo shehena zetu zilifika Sierra Leona kabla ya kutokea kwa ugonjwa wa Ebola. baada ya kutokea ugonjwa wa Ebola, shehena zetu zimesafirishwa kwa sehemu mbalimbali zinazokumbwa na ugonjwa huo, shehena zetu zimeonesha umuhimu mkubwa katika kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leona."

    Bw. Zou amejulisha kuwa, habari kutoka wizara ya afya ya Sierra Leone zinaonesha kuwa, hadi Jumanne wiki hii kesi 703 za Ebola zimethibitishwa nchini humo, ambao 259 kati yao wamefariki. Amesema, Kuna kesi 12 tu katika mji mkuu wenye idadi ya watu milioni 2, hali ambayo iso mbaya sana, wengi zaidi ni wale walioambukizwa katika sehemu nyingine nchini na kuja kutafuta matibabu.

    Inafahamika kuwa, madaktari wa kundi la matibabu la China nchini Sierra Leone wanaendelea na kazi zao kwa sasa. Jopo la pili la mali za misaada zenye thamani ya yuan milioni 10 zinazotolewa na China litawasili nchini Sierra Leone, huku mafunzo kuhusu matumizi ya mali husika yatatolewa na wataalamu wa usalama wa umma wa China kwa wafanyakazi husika wa Sierra Leone. Bw. Zou ameeleza, kutokana na juhudi hizo mbili, hali ya kinga na udhibiti dhidi ya maambukizi ya Ebola itaboreshwa zaidi.

    "Hivi sasa idadi ya walioambukizwa inaongezeka kwa watu 10 hadi 20 kila siku, lakini tunakadiria hilo huenda ni ongezeko kabla ya kufikia kikomo, ambalo litapungua hatua kwa hatua kadiri watu watakapotilia maanani zaidi kuhusu hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo pamoja na hatua za kinga na udhibiti husika zitakapotekelezwa zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako