Mtendaji mkuu wa ligi ya Primia Richard Scudamore amesema Luis Suarez ni "ajali inayosubiri kutokea". Suarez anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi mine baada ya kumn'gata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini katika kombe la dunia. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uruguay mwenye miaka 27, ambaye leo atajua hatma ya rufaa yake dhidi ya marufuku inayomkabili, ameondoka Anfield na kujiunga na Barcelona kwa ada ya pauni milioni 75. Hukumu ya rufaa yake itatolewa saa nane mchana wa leo pamoja na maelezo kamili ya uamuzi uliochukuliwa. Mawakili wake wanampango wa kuomba aruhusiwe afanye mazoezi na timu yake mpya katika kipindi hicho cha kufungiwa, na marufuku hiyo iwe kwa michezo ya kimataifa tu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |