• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaeleza wasiwasi wa Ebola nchini Nigeria kwa CAF

    (GMT+08:00) 2014-08-14 15:20:29

    Chama cha soka cha Rwanda kimeiandikia CAF juu ya wasiwasi wake kuhusu virusi vya Ebola nchini Nigeria. Rwanda imepangiwa kucheza na Super Eagles huko Calabar Septemba 6 katika michuano ya kufuzu ya kombe la mataifa ya Afrika. Rais wa chama hicho Vincent Nzamwita amesema pia chama chake kitapata maelekezo kutoka kwa serikali ya Rwanda, kama ikiamua Amavumbi wasiende Nigeria wataheshimu uamuzi huo. Hadi sasa watu watatu wameshafariki kwa Ebola nchini Nigeria, na kesi zote zinahusishwa na walaiberia watatu waliokwenda kutembelea Lagos Julai 25. Wakati huohuo Shirikisho la Soka barani Afrika limeiagiza Guinea kuandaa mechi baina yake na Togo katika taifa mbadala kufuati mlipuko wa Ugonjwa huo. Agizo hilo linamaanisha mechi baina ya timu hizo mbili zilizopangiwa kuchezwa kati ya tarehe 5-6 Septemba hazitachezwa huko. Aidha CAF imeagiza kuwa marufuku hiyo ya mechi nchini Guinea isalie hivyo hadi baada ya mwezi Septemba. Togo ilikuwa meiomba shirikisho la soka barani Afrika CAF kuhamisha mechi baina yake na Guinea kuenda taifa mbadala ikihofia usalama wa wachezaji wake kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako