Timu ya Uganda yenye wachezaji sita imeondoka jana kuelekea kwenye michezo ya 2 ya Olimpiki ya Vijana inayofanyika Nanjing China. rais wa kamati ya olimpiki ya Uganda William Blick amesema anatarajia wachezaji wake watafanya vizuri kwenye michezo hiyo. Michezo hiyo ambayo inawakutanisha pamoja wanariadha vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, itaanza tarehe 18 na kumalizika tarehe 28 mwezi huu. Katika michuano hiyo kutashindawa michezo kama ya uogeleaji, kupiga mbizi, badminton, mpira wa kikapu na mingineyo. Katibu mkuu wa baraza la taifa la michezo NCS, ametaka wanariadha kujitahidi ili kushinda medali .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |