• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha wa Kenya Edwin Kipchumba aanguka na kufa akiwa mazoezini

    (GMT+08:00) 2014-08-14 15:21:20

    Mwanariadha aliyeshiriki Olimpiki ya viziwi Edwin Kipkosegei Kipchumba, alianguka juzi asubuhi na kufa wakati akiwa kwenye mazoezi na wanariadha wenziwe katika barabara itokeayo Eldorent na kuelekea Kimunu. Kipchumba alikuwa mwanariadha wa kwanza wa Kenya kushinda medali ya dhahabu kwenye mchezo wa marathon katika olimpiki ya viziwi iliyofanyika mwaka 2005 huko Melbourne Australia. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la wanariadha wataalamu la Kenya Gilbert Kiplom, Kipchumba aliamka asubuhi na kuungana na weziwe kwenye mazoezi ya asubuhi ambapo wanakimbia km 20, kabla ya kukumbwa na umauti akiwa njiani. Amesema katika mazoezi hayo Kipchumba alikuwa katika kikosi cha mbele kinachoongoza na baada ya km 12 alisema anataka kupunguza kasi na baadaye alikwenda pembeni mwa barabara na kuanguka. Katika uhai wake Kipchumba pia alipata medali ya shabakwa kukimbia mita 3000, mita 5000 na mita 800 katika olimpiki ya majira ya joto huko Melbourne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako