• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufanya maandalizi kwa kupambana na ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-14 18:57:37

    Kampuni ya sayansi na teknolojia ya biolojia ya Jinweizhi ya Suzhou mkoani Jiangsu, China leo imetangaza kuwa imefanikiwa kuunganisha jini muhimu za virusi vya Ebola, na imekabidhi kituo cha udhitibi wa maradhi cha China. Jini muhimu za virusi vya Ebola ni msingi wa kufanya utafiti wa protini za viruri hivyo vinavyosababisha maradhi na muundo wake, ambao unasaidia kuelewa mapema tabia za virusi hivyo vya kusababisha ugonjwa na njia yake ya maambukizi..

    Aidha kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China inasema China imekuwa na uwezo wa kufanya utafiti na kutengeneza dawa ya kupima na kuthibitisha virusi vya Ebola, na imefahamu jini ya kinga ya virusi vya Ebola. Naibu mkuu wa idara ya elimu ya sayansi katika kamati hiyo Bw. Wang Chen amesema kwa sasa China imefanya maandalizi ya kiteknolojia kwa ajili ya mapambano dhidi ya virusi vya Ebola.

    "tumeshakuwa na uwezo wa kufanya utafiti na kutengeneza dawa ya kupima na kuthibitisha virusi vya Ebola, lakini kutokana na kutokuwa na mgonjwa, hatuwezi kufanya majaribio kwa wagonjwa."

    Bw. Wang Chen pia amesema China ina uwezo wa kutengeneza kinga za aina mbalimbali, ikipata jini ya kinga ya virusi vya Ebola, haitachukua muda mrefu kuanza utengenezaji wa kinga ya virusi hivyo.

    Habari nyingine zinasema, ingawa shirika la afya duniani limekubali kutumia dawa za majaribio katika tiba ya Ebola, lakini mtaalamu wa Marekani Bw. Anthony Fauci ametoa onyo kuwa kutumia dawa za majaribio mapema, huenda kutakuwa na athari mbaya. Anaona kuwa kwa sasa njia ya kutegemeka ni kueneza hatua zenye ufanisi za afya ya umma, na kutoa misaada ya kimataifa kwa nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako