Mamia ya mashabiki wa soka nchini Ghana wamefanya maandamano mjini Accra juzi ili kupinga uamuzi wa ubalozi wa Canada kukataa kutoa viza kwa maelfu ya mashabiki wanaotaka kwenda kuangalia michuano inayoendelea ya kombe la dunia kwa vijana wenye chini ya umri wa miaka 20 ya FIFA, licha ya kwamba wamefikisha vigezo vyote. Wajumbe wa makundi 30 ya umoja wa mashabiki walianza kuandamana katika uwanja wa Kwame Nkrumah, ingawa wawakilishi wa Ghana katika mashindano hayo Black Princesss, wamejitoa licha ya kuifunga Finland kwa mabao 2-1 mapema Jumatano. Hatimaye waandamanaji waliwasilisha maombi rasmi kwa serikali zote mbili, kupitia wizara ya mambo ya nje na ubalozi wa Canada wakidai walipwe fedha zao walizotumia kuombea viza na mambo mengine. Uamuzi wa ubalozi wa Canada kukataa maombi ya viza, unaaminika kutokana na ripoti kwamba zaidi ya mashabiki 200 wa Ghana waliokwenda kutazama kombe la dunia nchini Brazil, waliomba hifadhi ya kisiasa kwa kisingizio cha uongo kwamba kuna vita vya kikabila nchini Ghana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |