• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tiger ajitoa kwenye kombe la Ryder

    (GMT+08:00) 2014-08-15 15:51:35

    Tiger Woods amethibitisha kuwa hatashiriki kwenye kombe la Ryder mwezi ujao litakalofanyika huko Gleneagles, baada ya kujitoa kwenye mashindano ya kufuzu kwenye timu ya Marekani. Uamuzi huo ameutoa baada ya kushauriwa na madaktari na mkufunzi wake. Woods mwenye miaka 38, ambaye amekosa ziara ya msimu huu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo, amesema ameshauriwa apumzike kwani mgongo wake unahitaji kupona. Tiger amemfahamisha kocha wa timu ya Taifa ya Marekani Tom Watson kwamba kutokana na hali yake ya kiafya anajitoa na hataweza kuhudumia kama nahodha wa timu kwenye mashindano hayo na pia amemuomba amuwie radhi kwani wataalamu wake wa Afya wamemtaka apumzishe mgongo wake wenye matatizo na hata wamemzuia asifanye mazoezi yoyote. Mshindi huyo wa mara 14 amecheza mechi 33 za kombe la Ryder.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako