Sierra Leone imepanda hadi nafasi ya 14 katika viwango vya Fifa mwezi Agosti, na kuwafanya kupanda katika nafasi 50 kwa mara ya kwanza kwenye historia.The Leone Stars, ambao sasa wapo nafasi ya 50 duniani, pia wameingia katika 10 bora kwa bara la Afrika na kuchuku nafasi ya 7. Lakini Lesotho nayo pia imefanya vizuri duniani, ambapo wamepanda kwa nafasi 26 na kukamata nafasi ya 105, na katika Afrika wamechukua nafasi ya 29. Nayo Algeria imeendelea kuwa kwenye nafasi ya kwanza katika bara la Afrika. Kwa upande wa mwezi Julai nchi zilizokuwemo kwenye 10 bora za Afrika katika viwango vya Fifa ni kama ifuatavyo-:
1. Algeria, duniani wa 24,
2. Ivory Coast, duniani wa 25
3. Nigeria, duniani wa 33
4. Ghana, duniani wa 36
5. Misri, duniani wa 38
6. Tunisia, duniani wa 42
7. Sierra Leone, duniani wa 50
8. Cameroon, duniani wa 54
9. Burkina Faso, duniani wa 58 na
10. Senegal, duniani wa 59
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |